Mwandishi habari maarufu wa Pakistan,Arshad Sharif ameuwawa kwa kupigwa risasi kichwani usiku wa kuamkia leo katika barabara kuu ya Nairobi-Magadi nchini Kenya. Taarifa za awali zinasema Arshad Sharif aliuawawa baada ya yeye na dereva wake kukaidi amri ya kusimamisha gari lao kwenye kizuizi kilichokuwa kimewekwa kukagua magari.