Polisi nchini Kenya yawasaka Al-shabaab

Polisi nchini Kenya imeimarisha operesheni za usalama katika mji wa Mandera uliopo mkoa wa Kaskazini Mashariki mwa Kenya, na kuwasaka wapiganaji wa al-Shabaab waliovamia misikiti miwili na baadaye kutoa hotuba mbele ya waumini waliomo ndani kabla ya kuondoka.

Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Kaskazini Mashariki George Seda amesema, wapiganaji hao walibeba bunduki aina ya AK47 na kwenda kwenye misikiti ya Elram A na B wakati wa sala ya alfajiri Jumamosi na kuwaambia waumini waliokuwepo misikitini kuwa wapo kwenye vita na watu wasio waislamu na kuwataka wajiunge na vita hivyo. Kwa mujibu wa Seda hakuna aliyejeruhiwa kwenye tukio hilo.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii