Abiria Aenda Haja Kubwa Katika Ndege Mbele ya Wenzake

Kizaazaa kilishuhudiwa katika uwanja wa ndege wa Heathrow jijini London nchini Uingereza baada ya mwanamume kuvua nguo zake na kwenda haja kubwa katika ndege ya British Airways.


Kwa mujibu wa jarida la The Sun, abiria huyo ambaye alikuwa anaelekea nchini Nigeria alienda haja kubwa mbele ya wenzake muda mfupi tu kabla ya ndege hiyo ya Britisha Airways kupaa angani.
Baada ya kumaliza kudodosha kinyesi, abiria huyo alichukua kinyesi hicho na kuanza kujipaka mwilini kote kabla ya kuanza kupaka viti vya ndege na kuwaacha abiria wengine kwa mshangao na butwaa.


Wakati wa kuabiri, abiria mmoja alivua nguo kutoka kiunoni na kunya sakafuni. Aliketi kwenye kinyesi hicho na kukisugua kwa sakafu na kapeti. Alianza kukimbia hadi kwenye mlango wa nne na kupaka viko vyake na viti vya mlangoni kwa kinyesi," The Sun imenukuu taarifa ya British Airways.


Shirika la ndege la Britisha Airways lililazimika kubadili ndege ya kwenda safari hiyo huku hiyo iliyokuwa na kinyesi ikipelekwa kufanyiwa ukarabati na usafi kwa gharama kubwa kwa shirika hilo.
    "Tuliwaomba msamaha abiria wetu kwa kuchelewa kwa safari yao ya ndege na kuwapangai ndege nyingine ili kuwaruhusu kuendelea na safari yao," British Airways iliambia The Sun.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii