Zelenskyy" Urusi kutumia ndege zisizo na rubani za Iran kunaonyesha imefilisika kijeshi"

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy amesema Urusi kutumia ndege zisizo na rubani za Iran ili kuyashambulia maeneo ya Ukraine, kunaweka wazi kuwa Urusi imefilisika kisiasa na kijeshi licha ya miongo kadhaa ya uwekezaji katika sekta ya ulinzi.

Ukraine imebaini kuwa mashambulizi ya Urusi ya hivi karibuni kwenye miundombinu yake yamefanyika kwa kutumia ndege zisizo na rubani zilizopewa jina "kamikaze" zilizotengenezwa na Iran.

Kiev na washirika wake wa Magharibi wamekuwa wakiituhumu Iran kutoa ndege hizo. Utawala wa Tehran umekanusha madai hayo na kusema hayana msingi lakini wakibaini kuwa tayari kwa mazungumzo na Kiev. Urusi kwa upande wake imesema haikuwa na taarifa iwapo ndege hizo zilitumiwa au la.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii