Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amelaani mashambulizi mapya ya Urusi yaliohusisha makombora na ndege zisizo na rubani na kuyataja kama ugaidi dhidi ya raia.
Ndege hizo zisizo na rubani zilizotumiwa na Urusi zimepachikwa jina la kamikaze, kwa sababu zinaharibika baada ya kupiga shabaha. Rais Zelensky ameandika katika matandao wake wa Telegram kwamba adui anaweza kushambulia miji lakini hawezi kuidhoofisha Ukraine. Mamlaka ya mji mkuu Kyiv imetoa tahadhri kwa raia na kuwataka kutafuta hifadhi katika sehemu za kujilinda na mabomu haraka iwezekananvyo.
Aidha katika hatua nyingine mawaziri wa mambo ya nje wa Umoja wa Ulaya wanakutana ambapo uvamizi wa Urusi nchini Ukraine ni miongoni mwa masuala yanayojadiliwa. Mkuu wa sera za kigeni Jossep Borell anasema Urusi tayari imeshindwa kwenye uwanja wa mamapambano.Uvamizi wa Urusi nchini Ukraine ukiwa unakaribia miezi 8,Ukraine imeendelea kuomba uungwaji mkono kutoka kwa washirika wake wa magharibi.