Chanzo cha kifo cha Mchezaji Emiliano Sala Chafamika

rubani wa ndege iliyokuwa imembeba mwanasoka wa Argentina Emiliano Sala aliwaambia rafiki zake kuwa ndege ile ilikuwa na matatizo kabla haijapata ajali.Emiliano Sala


Sauti ya rubani David Ibbotson (59) imesikika ikisema ”nitavaa jaketi langu la kujiokolea nikiwa kwenye safari kutoka Ufaransa kwenda Wales,”

”Mara ya mwisho kuendesha hii ndege kuna kishindo nilikisikia, halafu pedeli ya breki ya kushoto haifanyi kazi, hii ndege ingerudishwa kwenye banda ikakae.”

Ndege hiyo ilipata ajali mwaka 2019 wakati Sala akitokea Nantes kuelekea kujiunga na Cardiff City baada ya kusaini mkataba wa pauni milioni 15.

Ibbotson ambaye alifariki pamoja na Sala kwenye ajali hiyo alikuwa ni rubani asiye na leseni ya kuendesha abiria wanaolipa.

David Henderson , mfanyabiashara aliyehusika kuandaa safari hiyo bila kibali anatumikia kifungo cha miezi 18 jela kwa kosa la kuweka usalama wa watu na ndege hatarini.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii