Korea Kusini na Marekani zarusha makombora baada ya jaribio la Korea Kaskazini

Korea Kusini na Marekani zimefyatua makombora manne ya ardhini kuelekea katika Bahari ya Mashariki, inayojulikana zaidi kama Bahari ya Japan.

Duru za kijeshi za Korea Kusini zimeeleza leo kuwa makombora hayo yamerushwa ikiwa ni katika kujibu jaribio la kombora la masafa ya kati lililofanywa na Korea Kaskazini jana kuelekea Japan.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo ya kijeshi, kila nchi ilirusha mfumo wa makombora mawili ya masafa mafupi aina ya ATACMS yaliyotengenezwa Marekani.

Aidha, jeshi la Korea Kusini limethibitisha kuwa kombora moja lililotengenezwa na Korea Kusini aina ya Hyunmoo-2 lilishindwa kuruka muda mfupi baada ya kufyatuliwa na kuanguka. Hata hivyo, kombora hilo halijasababisha madhara yoyote yale.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii