Mlemavu wa macho amuua mama yake

Bibi mwenye umri wa miaka 87 anayefahamika kwa jina la Elina Nzilano mkazi wa mtaa wa Idofi halmashauri ya mji wa Makambako mkoani Njombe ameuawa na mwanae mwenye ulemavu wa macho (Kipofu) anayefahamika kwa jina Elisha Mwena (42) huku sababu ikitajwa kuwa ni kikongwe huyo kumnyima chakula


Kwa mujibu wa ripoti ya awali ya jeshi la polisi inasema mlemavu huyo wa macho ambaye ni mtoto wa bibi huyo alikasirishwa na kitendo chake cha kumyima mwanae chakula na sabafubu kubwa ya kutompa chakula ni mjukuu wake kuiba kuku wake na kumla.

Akizungumzia tukio hilo kamanda wa jeshi la polisi Hamis Issa amesema Mlemavu huyo wa macho alimshambulia mama yake baada ya mtoto wake kutopewa chakula kwasababu ya kuiba kuku wa bibi huyo na kisha kumla jambo ambalo likamkasirisha na kisha kuanza kumpa kichapo kwa fimbo bibi huyo na kumsababishia kifo.



Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii