Kimbunga Ian kimeacha nyumba milioni mbili bila umeme na kuharibu miundo mbinu Florida

Kimbunga Ian kiliwasili magharibi mwa Florida Jumatano kama kimbunga cha 4 chenye upepo wa zaidi ya kilomita 240 kwa saa, na kusababisha mafuriko mabaya katika maeneo kadhaa.

Kimbunga Ian kilitua karibu na Cayo Costa, kusini-magharibi mwa peninsula, kama kimbunga ‘’hatari sana’’ saa 3:05 usiku kwa saa za huko (7:05 pm GMT), kulingana na Kituo cha Kitaifa cha Vimbunga cha Marekani

Kimbunga hicho kilisababisha dhoruba iliyopanda mita kadhaa kwenda juu ambacho kilifurika maeneo makubwa ya pwani ya kusini magharibi mwa Florida.

Zaidi ya nyumba milioni 2 hazikuwa na umeme katika jimbo lote, kati ya jumla ya milioni 11, huku maafa zaidi yakitarajiwa wakati dhoruba ikiendelea.

‘’Ni mojawapo ya vimbunga vitano vibaya zaidi kukumba eneo la Florida,’’ Gavana wa Florida Ron DeSantis alisema katika mkutano wa wanahabari Jumatano alasiri.

Anthony Reynes, mtaalam wa hali ya hewa katika NHC huko Miami, aliambia BBC kwamba dhoruba hiyo huenda ikawa ya kihistoria.

‘’Ni dhoruba kubwa na itachukua muda kudhoofika kadiri inavyoendelea kusonga.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii