Mahakama ya Wilaya ya Kiteto imemhukumu Amos Nyang’waji kifungo cha miaka minne jela au kulipa faini ya Sh1.2 milioni kwa kosa la kumchapa viboko karani wa Sensa ya Watu na Makazi aliyekuwa Kijiji cha Matui Wilayani humo akitekeleza majukumu yake.
Hukumu hiyo imetolewa jana Agosti 30, 2022 na Hakimu mkazi wa mahakama hiyo, Mosi Sasy.
Karani huyo alikuwa nyumbani kwa Andrea Nyang’waji wa Kijiji cha Matui Wilayani Kiteto mkoani Manyara, akitimiza majukumu yake.
Akisoma mashtaka mawili mbele ya Hakimu mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Kiteto, Mosi Sasy, Mwendesha Mashtaka wa Polisi, Joseph Jemes amesema tukio hilo lilitokea Agosti 25 mwaka huu katika Kijiji cha Matui wakati karani huyo akitekeleza majukumu ya Sensa ya Watu na Makazi.