Wapigakura Mombasa, Kakamega Wahimizwa Wajitokeze Kwa Wingi

Shughuli ya upigaji kura kuchagua gavana katika Kaunti ya Mombasa na Kakamega inaendelea.Vituo vilifunguliwa mapema Jumatatu, wakazi katika kaunti hizo wakijitokeza kurusha kura.Kaunti hizo uchaguzi kiti cha ugavana haukufanyika Agosti 9, 2022 kufuatia dosari zilizotambulika kwenye karatasi za kura – picha kukosa kuandamana na wagombea.Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) iliahirisha chaguzi hizo, zikaratabiwa kufanyika Agosti 23 kisha baadaye kuahirishwa tena kuwa Jumatatu, Agosti 26.Maeneobunge; Rongai katika Kaunti ya Nakuru, Kitui Rural na Pokot South, wenyeji pia wanashiriki kuchagua wabunge wao.

Idadi ya chini ya waliojitokeza hata hivyo imeripotiwa, mgombea wa ugavana Kakamega, Fernandes Barasa akisema wapigakura wanachelea wakilinganisha zoezi hilo kama lile ndogo.“Huenda wanachakulia shughuli hii kama chaguzi ndogo, ambapo idadi ndogo ya watu hujitokeza,” Bw Barasa akasema baada ya kupiga kura katika kituo cha Matungu.

Barasa aidha amehimiza wapigakura kujitokeza kwa wingi, kushiriki zoezi hilo la kidemokrasia.Mwaniaji huyo wa ODM anamenyana na seneta wa Kakamega, Cleophas Malala (Amani National Congress – ANC).

 


Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii