Waasi nchini Burkina Faso waua watu 6

Watu wenye silaha na wasiojulikana wamewaua watu sita na kuwajeruhi wengine wawili katika shambulio dhidi ya msafara kutoka mgodi wa dhahabu wa Boungou mashariki mwa Burkina Faso. Taarifa ya Jeshi imefahamisha kuwa, wiki iliyopita, magari matano yalitumwa kutoka katika mgodi unaomilikiwa na kampuni ya kuchimba madini ya Endeavor , ili kuusaidia msafara mwengine ambao ulikuwa umekwama kwenye tope kwa siku kadhaa. Shambulio hilo linadhihirisha jinsi ilivyo hatari ya kufanya kazi nchini Burkina Faso, ambapo tangu mwaka 2018 wanamgambo wenye itikadi kali za Kiislamu wenye mafungamano na Kundi linalojiita Dola la Kiislamu IS na al Qaeda, wamechukua udhibiti wa maeneo makubwa ya kaskazini na mashariki mwa nchi hiyo, na kusababisha vifo vya maelfu ya watu na kuwalazimu wengine zaidi ya milioni moja kuyahama makazi yao.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii