Pakistan inaomba msaada zaidi wa kimataifa baada ya mafuriko kusababisha uharibifu mkubwa kote nchini humo.
Marekani, Uingereza, Umoja wa Falme za Kiarabu na nchi nyingine zimechangia kusaidia madhara ya maafa ya monsuni lakini fedha nyingi zaidi zinahitajika, afisa wa wizara ya mambo ya ndani
Zaidi ya watu 1,000 wamefariki katika mafuriko hayo na mamilioni ya wengine wamekimbia makazi yao tangu Juni, Salman Sufi alisema.
Alisema serikali ya Pakistan inafanya kila iwezalo kusaidia watu.
Waziri Mkuu wa Pakistan Shehbaz Sharif alisema watu milioni 33 wamekumbwa na mafuriko - karibu 15% ya idadi ya watu nchini humo.
Alisema hasara iliyosababishwa na mafuriko msimu huu ni sawa na ile ya wakati wa mafuriko ya 2010-11, ambayo inasemekana kuwa mbaya zaidi katika rekodi.
Maafisa nchini wanalaumu mabadiliko ya hali ya hewa kwa uharibifu huo. Lakini mipango duni ya serikali za mitaa pia imetajwa kuwa sababu ambayo imezidisha hali ya mafuriko huko nyuma, na majengo mara nyingi yanajengwa katika maeneo yanayokumbwa na mafuriko ya msimu.