MAPACHA WAOA MKE MMOJA.

Teddy na Peter amabao ni mapacha wako katika uhusiano wa mapenzi na mwanamke mmoja kwa jina Emily ambaye wanadai ni mke wao
Uhusiano huo wa kushangaza umempelekea Emily kupata mimba na amefichua kuwa hafahamu ni nani kati ya mapacha hao ndiye baba halisi wa mwanaye
Emily, Teddy na Peter walisimulia kuwa walikutana katika hafla ya kanisa na kuanza kuchumbiana baada ya kubadilishana nambari za simu
Mapacha wawili wamezua mjadala mtandaoni baada ya kufichua kuwa wamemuoa mke mmoja na wanatarajia kupata mtoto hivi karibuni.

Mapacha Wakorino Waoa na Kumpachika Mimba Mke Mmoja: "Tunalala Kitandani Kimoja"
Mapacha Wakorino Waoa na Kumpachika Mimba Mke Mmoja. Picha: Nicholas Kioko.
Watatu hao wakiwa wamevalia kofia za Akorino na mashati yanayofanana, waliwaacha wengi vinywa wazi baada ya kufichua kuwa wanalala kitanda kimoja.

Katika video kwenye Youtube iliyopakiwa na mwanablogu Nicholas Kioko, watatu hao walisema wanapendana sana.

Mapacha hao, Teddy na Peter walidai kuwa hawajafunga ndoa rasmi na Emily ingawa wanaishi nyumba moja na hivi karibuni wanatarajia kuitwa baba.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii