Watu 6 Wapoteza Maisha kwa Kukatwa Vichwa na Waasi Nchini Msumbiji

RAIS wa Msumbiji Fillipe Nyusi amesema wanamgambo wa kiislamu walioasi katika jimbo la Napula wamewakata vichwa watu sita (6) huku wakiwateka nyara watu wengine watatu.

 

Wakati akizungumza mubashara kupitia Televisheni ya kitaifa akiwa kwenye Jimbo la Kusini la Gaza, Nyusi amethibitisha tukio hilo akiongeza kwamba idadi kubwa ya nyumba pia zilichomwa.


Hilo ndilo shambulizi la tatu kufanyika mkoani Nampula ndani ya kipindi cha siku 5, hali ambayo imesababisha wimbi jipya la watu wanaotoroka makwao, ingawa idadi kamili haijulikani.

 

Nyusi amesema kwamba imekuwa vigumu kwa vikosi vyake kuwasaka magaidi kutokana na kuwa wanajificha kwenye misitu mikubwa baada ya kufanya mashambulizi.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii