50 Wanusurika Kifo Basi Likiteketea kwa Moto

Basi la kampuni ya usafirishaji la Tashrif limeteketea kwa moto asubuhi ya leo tarehe 16 Agosti 2022 wakati likiwa safarini kutoka Tanga Mjini kuelekea Masasi mkoani Mtwara.

 

Dereva wa Basi hilo alisema ya kuwa walilichunguza basi hilo kabla ya safari na hawakuona tatizo lolote, hivyo chanzo cha ajali hiyo ya moto hakikusababishwa na uzembe wao wa kutokagua basi kabla ya safari. Alisema hitilafu ilitokea ghafla tu.

 

Jeshi la zimamoto lilifanikiwa kufika katika eneo la tukio kuzima moto huo ingawa hawakufanikiwa kuokoa chochote kutoka kwenye basi hilo.

 

Hakuna kifo kilichoripotiwa kutoka kwenye ajali hiyo, abiria baadhi wamepata majeraha kidogo wakati wakiruka kupitia madirishani wakijaribu kuokoa maisha yao baada ya moto kutanda ndani ya basi hilo.

 

Tukio hili linatokea siku chache baada ya basi jengine la kampuni ya usafirishaji ya skyline nalo kuteketea kwa moto likiwa safarini.

 

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii