Naibu Waziri wa Ushirikiano wa Kiuchumi na Maendeleo wa Ujerumani atembelea Tanga

Naibu Waziri wa Ushirikiano wa Kiuchumi na Maendeleo wa Ujerumani Dr Bärbel Kofler, amefanya leo ziara ya kihostoria katika jiji la Tanga nchini Tanzania. Ziara yake inaleta ujumbe mzito wa uungwaji mkono wa serikali ya Ujerumani katika sera ya maendeleo ya wanawake ambayo inatambua na kuunga mkono kuendeleza huduma bora za afya kwa wanawake na watoto wachanga ambalo ni sharti la maendeleo endelevu, amani na jamii shirikishi. Dr.Kofler amepokelewa na Waziri wa Afya Ummy Mwalimu na kusindikizwa na viongozi wa mashirika ya Kijerumani ya maendeleo yaliyopo nchini Tanzania. Ujerumani kwa muda mrefu imekuwa ikiisaidia serikali ya Tanzania kuimarisha ujuzi wa wahudumu wa afya, kutoa vifaa muhimu, na kusaidia kuboresha upatikanaji wa huduma bora za afya kupitia bima ya afya ya taifa na kuweka mifumo ya afya kidijitali.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii