Takriban watu 52 wamefariki dunia

Sudan ilikumbwa na mafuriko katika wiki za hivi karibuni. Kulingana na Baraza la Kitaifa la Ulinzi wa Raia, watu 52 wamefariki dunia tangu mwezi Mei mwaka jana, mwanzoni mwa msimu wa mvua. Zaidi ya nyumba 8,000 zimebomoka au kuharibiwa. Idadi ya watu waliofariki dunia kutokana na mafuriko hayo inaweza kuongezeka katika wiki zijazo.


Msimu wa mvua nchini Sudan kwa ujumla huanzia mwezi Mei hadi Oktoba na mara nyingi mvua nyingi hunyesha kati ya mwezi wa Agosti na Septemba.

Idadi ya waathiriw inaongezeka kwa kasi , kama inavyobainishwa na shirika la Umoja wa Mataifa la Kuratibu Masuala ya kibinadamu na misaada ya dharura, OCHA. Kulingana na takwimu iliyosasishwa mara kwa mara kutoka kwa shirika hilo, idadi ya watu walioathiriwa imepungua kutoka 38,000 hadi 136,000 katika wiki moja, kulingana na hesabu za hivi punde za Jumatatu, Agosti 15. Na kuna baadhi ya maeneo ambapo ni vigumu kufika na ripoti huwafikia wahusika kwa kuchelewa.

Shirika hilo pia linahofia athari zisizo za moja kwa moja za mafuriko haya. Maisha ya Wasudan yanatishiwa moja kwa moja, mashamba na vyanzo vya maji kama vile visima vimezamishwa katika maeneo mengi ya nchi.

OCHA bado inajitahidi kutathmini uharibifu katika majimbo yaliyoathiriwa zaidi, ambayo ni Darfur Magharibi na Darfur ya Kati ambako waathiriwa yanatoa wito kwa mashirika ya kibinadamu kuwapa misaada.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii