Israel yamuua Mpalestina mmoja huko Jerusalem

Polisi wa Israel wamempiga risasi na kumuua Mpalestina mmoja aliyefahamika kwa jina la Mohammed al-Shaham ambaye alijaribu kuwashambulia maafisa hao kwa kisu wakati wakifanya msako wa silaha zinazomilikiwa kinyume cha sheria mashariki mwa Jerusalemu katika kitongoji cha Kafr Aqab. Tukio hilo linajiri siku moja baada ya Mpalestina mwengine kufanya shambulio la ufyatuaji risasi kwenye basi nje kidogo na mji wa kale wa Jerusalem na kuwajeruhi watu wanane wakiwemo raia wa Marekani. Vurugu hizo zinafuatia wiki ya ghasia kati ya Israel na wapiganaji wa Palestina kwenye ukanda wa Gaza na katika Ukingo wa Magharibi, zilizopelekea Wapalestina 49 wakiwemo watoto 17 kuuawa. Makubaliano ya usitishwaji mapigano yaliafikiwa chini ya usimamizi wa serikali ya Misri.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii