Wanajeshi watatu wauawa katika shambulio la anga karibu na Damascus

Jeshi la Israel limelaumiwa na vyombo vya habari nchini Syria kuhusika na mashambulizi ya anga karibu na mji mkuu Damascus na kusababisha vifo vya wanajeshi watatu na wengine kadhaa kujeruhiwa. Wakati huo huo, mkoa wa Tartus ulishambuliwa pia. Jeshi la Israel halikuzungumzia taarifa hizo ingawa limekuwa likishambulia mara kwa mara maeneo kadhaa katika nchi jirani ya Syria, ambayo bado inakabiliwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe. Lengo la kimkakati la Israel ni kuzuia adui yake mkuu Iran na wanamgambo wake kupanua ushawishi wao wa kijeshi nchini Syria. Pamoja na Urusi, Iran ndio mshirika mkuu wa serikali ya Syria katika vita hivyo.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii