Mafuriko yaliyosababishwa na mvua za msimu nchini Sudan yamesababisha vifo vya zaidi ya watu 50 na kuharibu makazi zaidi ya 8,170 tangu kuanza kwa msimu huo wa mvua.Msemaji wa kitengo cha taifa cha kuwalinda raia nchini Sudan, Brigedia Jenerali, Abdul-Jalil Abdul-Rahim amesema vifo 19 vimetokea jimbo la Kordofan Kaskazini, ikifuatiwa na jimbo la Mto Nile ambalo limerekodi vifo 7.Hata hivyo hakusema lini hasa vifo vya mwazo vimetokea. Lakini msimu wa mvua nchini Sudan kwa kawaida unaanzia mwezi Juni hadi Septemba, na mafuriko yanakuwa ya kiwango cha juu katika miezi ya Agosti na Septemba.