Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro, Lengai Ole Sabaya na wenzake wanne wamefikishwa tena katika mahakama ya hakimu mkazi Moshi leo Agosti 12.
Sabaya na wenzake wanakabiliwa na mashitaka saba yakiwemo ya uhujumu uchumi, utakatishaji fedha, matumizi mabaya ya ofisi pamoja na rushwa ya Sh30 milioni kutoka kwa mfanyabishara wa Bomang'ombe, Alex Swai.
Washatakiwa wengine katika kesi hiyo namba 2 ya mwaka 2022, ni pamoja na Sylvester Nyegu, John Aweyo, Nathan Msuya na Antero Assey.
Sabaya alifikishwa kwa mara ya kwanza katika mahakama hiyo Juni Mosi mwaka huu, ambapo awali kesi hiyo ilikuwa mbele ya hakimu mkazi Mfawidhi, Salome Mshasha.