Wachimba migodi haramu washambuliwa Afrika Kusini

Maelfu ya waandamanaji wenye hasira nchini Afrika Kusini waliwasaka wachimba migodi wasiokuwa na vibali baada ya ubakaji wa wanawake wanane wiki iliyopita. Ubakaji huo ulifanyika katika mji wa Krugersdorp, Magharibi mwa Johannesburg. Waziri wa polisi Bheki Cele amesema kuwa wachimba migodi hao haramu almaarufu ''zama zamas" huenda walihusika katika shambulio hilo. Wachimba migodi hao kwa kiasi kikubwa ni wahamiaji wasio na vibali. Makundi ya wakazi walifunga mabanda na kuchoma nyumba katika jaribio la kuwafurusha wachimba migodi wanaoendeleza shughuli zao kinyuma cha sheria . Maafisa wa polisi walikaa mbali na kurusha maguruneti kutoka kwa helikopta ili kuwatawanya watu hao. Mamlaka imesema kuwa watu 29 walikamatwa kwa tuhuma za uhamiaji haramu. Polisi imesema uchunguzi wa mauaji ulifunguliwa baada ya mwili wa mwanamume mmoja kupatikana karibu na eneo hilo asubuhi. Haijabainika mara moja ikiwa kifo hicho kilihusishwa na maandamano hayo

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii