MBUGE AMUUA MPINZANI WAKE

Mbunge mteule wa Kimilili Didmus Barasa amekana mashtaka ya kumuua mlinzi wa mpinzani wake siku ya uchaguzi mkuu mapema mwezi huu.

Mbunge huyo alikuwa amefikishwa mbele ya mahakama ya Kakamega ambapo uamuzi wa dhamana ulipangwa kutolewa 3pm.

Barasa ambaye amekuwa chini ya ulinzi wa polisi kwa muda wa wiki mbili zilizopita anasemekana kutenda kosa hilo dhidi ya Brian Olunga, mpambe wa mwanasiasa wa Kimilili Brian Khaemba siku ya uchaguzi.

Alikuwa amezuiliwa katika seli za Kisumu ambapo alifikishwa kortini kwa karibu na mahakama iliruhusu polisi kumzuilia kwa wiki mbili kabla ya kujibu mashtaka.

Hii ilikuwa kuruhusu polisi kufanya uchunguzi wa mwili wa marehemu na kukusanya ushahidi mwingine unaohitajika kwa kesi hiyo.

Pia alipelekwa kufanyiwa uchunguzi wa kimatibabu ambapo maafisa walisema ni timamu na angejibu katika mahakama ya Kakamega.

Uchunguzi wa mwili wa Olunga ulionyesha aliaga dunia kwa jeraha la risasi ya bastola iliyompiga upande wa kulia wa kichwa chake.


Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii