MWANAUME AJIKATA SEHEMU ZAKE ZA SIRI AKIWA USINGIZINI.

Mwanamume mmoja kutoka taifa la Ghana anaendelea kupokea matibabu hospitalini baada ya kujikata sehemu zake za siri kwa bahati mbaya akilala.

Kofia Atta mkulima mwenye umri wa miaka 47 alisema kuwa alikata sehemu ya kende lake baada ya kulala akiwa kwenye kiti alikoota kuwa alikuwa anakata kipande cha nyama.

“Nilikuwa nimeketi kwa kiti change niliposhikwa na usingizi na kulala. Usingizini, niliota kuwa nilikuwa nakata kipande cha nyama mbele yangu. Sikumbuki nilivyochukua kisu. Atta aliaambia runinga ya BBC News Pidgin.

Majirani waliosikia mayowe yake ya kutaka msaada walidhani kuwa alikuwa akishambuliwa na kukimbia nyumbani kwake ili kumwokoa.

alipofika, walimpata akiwa pekee yake chumbani huku akibubujika damu. Walimkimbiza hospitalini ambako bado anapokea matibabu.

Atta sasa anasema kuwa anatafuta msaada wa wahisani kupata fedha zinazohitajika ili kufanyiwa upasuaji alivyoelekezwa na madaktari katika hospitali hiyo.

“Kwa sasa niko katika hospitali hii. Walichonipatia ni maji na kudungwa lakini nahitaji kufanyiwa upasuaji. Sina pesa za kuweka mafuta kwenye gari la wagonjwa ili linipeleke katika Hospitali ya Mafunzo ya Komfo Anokye kwa ajili ya upasuaji,” Atto alisema.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii