Kampeni za uchaguzi wa rais nchini Brazil zazinduliwa rasmi

Kampeni za uchaguzi wa rais nchini Brazil zinaendelea huku rais wa zamani Luiz Inacio Lula da Silva akiongoza kura za maoni ya umma dhidi ya rais aliyeko madarakani Jair Bolsonaro.


 Luiz Inacio Lula da Silva

Da Silva ambaye aliitawala Brazil kwa mihula miwili kati ya mwaka 2003 hadi 2010 alifungua kampeni yake rasmi jana ya kuwania tena wadhifa huo kwa mkutano kwenye kiwanda kimoja cha kutengeneza magari nje kidogo ya mji wa Sao Paulo. Kwa upande wake rais Bolsonaro alihutubia mkutano wake wa kwanza wa kampeni katika mji wa Juiz de Fora, eneo ambalo alishambuliwa kwa kisu na mtu mwenye matatizo ya akili wakati wa kampeni za uchaguzi wa mwaka 2018. Kulingana na matokeo ya kura za maoni ya umma yaliyochapishwa siku ya Jumatatu, Lula anaongoza kwa asilimia 44 dhidi ya Bolsonaro mwenye asilimia 32 lakini wapiga kura wa Brazil watafanya uamuzi rasmi katika uchaguzi wa Oktoba 2.
Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii