Mgombea urais wa Kenya Kwanza William Ruto amejipata tena pabaya kwa kutoa matamshi yanayodhaniwa kuwa ya kudhalilisha kuhusu Gavana wa Kitui Charity Ngilu.
Naibu Rais alikuwa kwenye kampeni katika kaunti ya Kitui alipouliza yuko wapi Ngilu.
Hata hivyo, aliacha hotuba yake na kuanza kutilia shaka ndoa yake.
"Na yule mama (akiashiria Ngilu) alienda aje?" Ruto aliuliza umati uliofika kumsikiliza
Hapo ndipo sehemu ya umati ilipojibu kwa kelele: “Alienda Bondo”.
Naibu rais kisha akauliza: "Aliendaje Bondo, mlimnyima kura?"
Swali la Ruto linarejelea hatua ya Ngilu kujiondoa kwenye kinyang’anyiro cha ugavana Kitui.Mtu mmoja katika umati alijibu kwa sauti ya juu: "Aliolewa Bondo".
Bondo ndiko nyumbani kwa kiongozi wa chama cha ODM Raila Odinga. Ngilu, mkosoaji mkubwa wa Ruto, anamuunga mkono Raila kuwania urais.
Mtu mmoja katika umati alijibu kwa sauti ya juu: "Aliolewa Bondo".
Bondo ndiko nyumbani kwa kiongozi wa chama cha ODM Raila Odinga. Ngilu, mkosoaji mkubwa wa Ruto, anamuunga mkono Raila kuwania urais.
Hapo ndipo naibu rais alipojibu maoni hayo ya nasibu kwa kuuliza: "Kwani mama mzee hivi anaweza kuolewa? Ataolewa na nani?".
Matamshi hayo yamezua hisia kali miongoni mwa Wakenya kwenye mitandao ya kijamii huku baadhi wakidai naibu rais alimkosea heshima gavana huyo.