Uchaguzi wa Kenya watumbua upya makovu ya ufisadi

Waziri wa mambo ya ndani nchini humo Fred Matiangi ameeleza kwamba wagombea viti vya ubunge wanawahonga wapiga kura walioko vijijini kwa kuwapa hata shilingi 100 pekee kama njia ya kuwashawishi kuwapigia kura ili washinde kwenye uchaguzi huo.

Tume Huru ya Mipaka na Uchaguzi (IEBC) ambayo imefadhiliwa kidogo, lakini ambayo ilitaka kupunguza kiwango cha fedha ambazo wanaowania urais wanapaswa kutumia kwenye kampeni zao isipindukie bilioni 4.4, imewashutumu baadhi ya wanasiasa kwa kununua vitambulisho vya baadhi ya wananchi ili kuwazuia wasiwapigie kura washindani wao.

Si hayo tu, kati ya watu 214 walioorodheshwa na tume ya Maadili na kupambana na ufisadi kama waliokosa maadili na hawafai kuwa maafisa wa umma; tume ya uchaguzi iliwazuia sita pekee. Hayo yalisemwa mwezi Juni, na shirika la kupambana na ufisadi Transparency International na mashirika mengine yanayopambana na rushwa. Kuhusu wengine wote waliosalia kwenye orodha hiyo, tume ya IEBC ilishindwa kuwazuia. 

Vita dhaifu dhidi ya ufisadi

Rais ambaye muhula wake madarakani unafikia ukingoni Uhuru Kenyatta, amekemea ufisadi na kutaka uwazi, lakini amefanya kidogo katika kuwezesha hilo katika muongo mmoja aliokuwa madarakani.

Wagombea wawili wakuu wa urais kwenye uchaguzi huo, naibu rais William Ruto mwenye umri wa miaka 55 wa chama cha muungano wa Kenya Kwanza, na Raila Odinga mwenye umri wa miaka 77 wa muungano wa Azimio la Umoja, wamesema watapambana na ufisadi. Lakini kulingana na mashirika yasiyo ya serikali yanayosikitishwa na hali ya Kenya kushindwa kuangamiza ufisadi unaoyaangamiza maisha ya raia kila siku, hizo zinasalia kuwa ahadi tu.

Nchini Kenya, wagombea viti vya kisiasa hawana ulazima kuweka bayana matumizi yao ya fedha za kampeni. Hata hivyo wananchi wameshuhudia wanasiasa wakitumia helikopta na misafara mirefu ya magari wakifanya kampeni nchi nzima kwa miez

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii