Wanafunzi tisa wa Chuo Kikuu cha Moi nchini Kenya wanashikiliwa na polisi kwa tuhuma zinazosemekana za kusambaza jumbe za kumchafua mgombea wa urais kwa tiketi ya Kenya Kwanza Naibu Rais William Ruto.
Hakimu Mkazi wa Eldoret, Onkoba Mogire ameagiza wanafunzi hao washikiliwe katika kituo cha polisi cha Langas kwa siku tatu huku uchunguzi ukiendelea ambapo kesi hiyo itasomwa tena Agosti 5.
Hatua hiyo imekuja baada Ruto kujitokeza hadharani kulaani uwepo wa vipeperushi vyenye ujumbe wa kumchafua kwenye eneo la Eldoreti na maeneo mengine nchini humo.