Moto mkubwa unaoteketeza misitu washindwa kudhibitiwa California

Maafisa wanaokabiliana na moto mkubwa  unaoendelea kuteketeza misitu Carlifonia, wanakumbana na hali ngumu  kutokana na radi pamoja na joto la hali ya juu, vinavyoongeza moto kusambaa, huku wakifanya kila juhudi kulinda jamii.

Msemaji wa idara ya kitaifa ya misitu, Aderienne Freeman, amesema kwamba moto mkubwa unaendela kuteketeza sehemu za Mckinney, katika msitu wa kitaifa wa Klamath, North Carolina.

Ukubwa wa moto huo umeongezeka na kuenea hadi umbali wa kilomita 207 mraba, siku mbili baada ya kuripotiwa katika kaunti ya Siskiyou, yenye idadi ndogo ya watu.

Uchunguzi unaendelea kubaini kilichosababisha moto huo.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii