Sabaya atinga mahakamani.

Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya na wenzake wanne wamefikishwa katika mahakama ya hakimu mkazi Moshi huku akiwa amefungwa bandeji kichwani.

Sabaya na wenzake wanakabiliwa na mashitaka saba likiwamo kosa la uhujumu uchumi, kuongoza genge la uhalifu, pamoja na kujihusisha na vitendo vya rushwa.

Kesi hiyo awali ilikuwa inasikilizwa na Hakimu Mfawidhi Mkazi, Salome Mshasha.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii