Polisi ya Tunisia imewazuia mamia ya waandamanaji kufika katika ofisi za tume ya uchaguzi, wakati waandamanaji wakimiminika barabarani kupinga kura ya maoni juu ya katiba mpya yenye utata ambayo itatoa fursa ya kupanua mamlaka ya utendaji ya rais. Waandamanaji hao wakiongozwa na kiongozi wa chama huria cha katiba Abir Moussi waliimba nyimbo za kupinga utawala wa kiimla na kushinikiza kuvunjwa kwa tume ya uchaguzi. Rais Kais Saied alipendekeza katiba mpya hivi karibuni ambayo ingepunguza majukumu ya bunge na badala yake kumuongezea mamlaka zaidi. Rasimu hiyo ya katiba itapigiwa kura ya maoni Julai 25, kura ambayo vyama vingi vya kisiasa vimeipinga. Saied ametawala kwa amri ya rais tangu kuanza kwa msimu wa kiangazi baada ya kulivunja bunge, kumfuta kazi waziri wake mkuu na kujiongezea mamlaka. Wakosoaji wake wameitaja hatua hiyo kama mapinduzi.