Maziko ya Vijana 21 waliofariki ndani ya klabu kufanyika leo

Ibada ya pamoja ya maziko ya vijana 21, waliofariki katika mazingira tatanishi kwenye klabu moja nchini Africa kusini, inafanyika leo.


Ibada  ya vijana hao wanaodaiwa kuwa na umri wa kati ya miaka 13-17, inafanyika katika bustan ya Scenery, mashariki mwa jiji la London.

Rais wa Africa Kusini ,Cyril Ramaphosa, maafisa wa serikali na mafariki ni baadhi ya wageni 3,000 wanaotarajiwa kuhudhuria mazishi ya leo.

Hakuna taarifa rasmi ambayo imetolewa kuhusiana na chanzo kamili cha vifo vya vijana hao wanaodaiwa kufariki wakati wakisherekea kumalizika kwa mitihani yao.

Hata hivyo uchuguzi wa awali umebaini kuwa huenda vijana hao walivuta hewa yenye sumu.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii