Mvulana wa Darasa la Nane Amuua Mama Mjamzito na Wanawe Wawili

Huzuni umeghubika kijiji cha Poroko katika kaunti ndogo ya Trans Mara Magharibi baada ya mvulana wa darasa la nane kumuua kinyama mwanamke mjamzito na watoto wake wawili.
Mvulana wa Darasa la Nane Amuua Mama Mjamzito na Wanawe Wawili.
Kulingana na polisi, mshukiwa huyo mwenye umri wa miaka 17, alimuua mwanamke huyo kwa kumdunga kisu kichwani, kifuani na sehemu nyingine za mwili.
Kisha aliwaua watoto wake wawili kwa kugeuza shingo zao kabla ya kutupa miili yao katika shamba la mahindi lililo mbali na nyumbani kwao.
Jamaa na majirani wa mshukiwa walibaini kuwa huenda kulizuka tofauti kati ya mshukiwa na marehemu kabla ya kuzua mashambulizi.
Polisi walithibitisha kuwa kijana huyo alikuwa akitumikia kifungo cha nje kwa kuiba redio, vikombe na sahani kutoka kwa marehemu anayesemekana kuwa halati wake.
Kwa kuwa kumfunga mpwa wake kunaweza kuhatarisha uhusiano wake na jamaa wa karibu, mwanamke aliyeuawa aliwasihi polisi wasimfunge mshukiwa.
“Naelewa kijana huyo anatoka kwa jirani tu, naambiwa alishukiwa kumuibia marehemu wakati fulani."
"Inashangaza kwamba nyumba hii italazimika kuzika watu wanne kwa sababu hospitali imethibitisha kuwa wataondoa mtoto ambaye hajazaliwa na kuzikwa kando. Hiki ni kitendo cha uhalifu na hatuwezi kukielezea kwa maneno mengine," Dominic Olonana, mkazi wa eneo hilo," alisema.
Majirani na jamaa waliobaini kuwa mvulana huyo alikuwa mhalifu mashuhuri pia waliambia polisi kuwa visa vya uhalifu vilikumba eneo hilo hivi majuzi.
Kwa sasa wamewataka polisi kuzidisha msako wa kuwasaka wahalifu ili kurejesha hali ya usalama na utulivu katika kijiji hicho.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii