Zelenskiy akiri kuondoka kwa majeshi ya Ukraine Lysychansk

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy amekiri kuondoka kwa vikosi vya nchi yake katika mji wa Lysychansk mashariki mwa jimbo la Donbass baada ya kuzidiwa nguvu na majeshi ya Urusi. Zelenskiy lakini ameahidi kwamba watauchukua tena udhibiti wa eneo hilo kwa kusaidiwa na silaha za mataifa ya Magharibi za kurusha makombora ya masafa marefu. Urusi imesema kuuteka mji wa Lysychansk chini ya wiki moja baada ya kuuteka mji wa Severodonetsk sasa umeipa udhibiti kamili wa eneo la Luhansk magharibi. Urusi inahisi kwamba huu ni ushindi wa kisiasa unaoendana na malengo ya nchi hiyo katika hivyo vita na Ukraine. Mapambano sasa yanaelekea katika eneo jirani la Donetsk ambalo majeshi ya Ukraine bado yana udhibiti mkubwa.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii