Urusi yaanza tena mashambulizi nchini Ukraine

Urusi jana ilianzisha tena mashambulizi yake katika eneo la Donbass Mashariki mwa Ukraine baada ya mapumziko ya muda mfupi ili kupanga tena vikosi vyake. Wakati wa ukaguzi wa vikosi vilivyohusika katika uvamizi nchini Ukraine, waziri wa ulinzi wa Urusi Sergei Shoigu, aliagiza mashambulizi ya kasi ya juu. Shoigu alitoa maagizo ya kupanua shughuli za makundi ya jeshi la nchi hiyo katika pande zote za mashambulizi.Wizara ya ulinzi ya Urusi imesema lengo ni kuzuia Ukraine kufanya mashambulizi makubwa ya makombora na silaha dhidi ya miundombinu na raia katika eneo la Donbas na maeneo mengine. Jeshi la Ukraine limeripoti kuwa limetibua jaribio la mashambulizi ya Urusi kuelekea Bakhmut na karibu na Donetsk katika muda wa masaa 24 yaliyopita. Mkuu wa jeshi la Ukraine pia amesema baada ya vikosi vya Urusi kujipanga tena, Urusi ilianzisha mashambulizi dhidi ya mtambo wa umeme wa Vuhlehirsk na kwamba mapigano yanaendelea.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii