Polisi Kariakoo Wapiga Jogging na Wananchi

JESHI la Polisi Wilaya Kipolisi ya Kariakoo, jijini Dar jana Jumamosi limefanya jogging na wananchi wa eneo hilo kumalizia na bonge la tizi wakihamasisha uzalendo na kuimarisha afya zao.

Jogging hiyo iliongozwa na Mkuu wa Upelelezi wa Wilaya ya Kipolisi ya Kariakoo, Afande OC-CID, Dr. Ezekiel Kyogo pamoja na maofisa wengine wa jeshi hilo kutoka wilaya hiyo.


ogging ilianzia Kituo cha Polisi cha Msimbazi na kuzunguuka Barabara ya Msimbazi kuelekea Barabara ya Morogoro ambapo walipofika makutano ya Barabara ya Bibi Titi na Morogoro walikunja kulia kuelekea Mnazi Mmoja mpaka Barabara ya Nyerere na kupiga jogging mpaka kwenye makutano ya Barabara ya Kilwa na Msimbazi maarufu kama mataa ya Kamata ndipo walinyoosha mpaka ‘Round about’ ya Shule ya Uhuru na kurudi Kituo cha Polisi Msimbazi ambapo walimalizia na mazoezi ya viungo.

Baada ya mazoezi hayo maofisa hao wa polisi wakiongozwa na OC-CID Dr. Ezekiel walianza kutoa elimu ya uzalendo ambayo ilikuwa ikisisitiza wanajamii kuipenda nchi hiyo.


Akizungumza na washiriki wa jogging hiyo, Dr. Kyogo aliwataka wafanya joggig popote nchini kuachana na kuimba nyimbo zisizokuwa za uzalendo kama ilivyo sasa ambapo wafanya jogging wengi wamekuwa wakitumia nyimbo za matusi badala ya nyimbo za kizalendo kama ilivyokuwa zamani.

Pia Dr Kyogo amewataka wanajamii wa maeneo hayo kushirikiana na jeshi la polisi kwa ajili ya kuendelea kudumisha usalama wa Kariakoo kama ilivyo sasa ambapo Kariakoo imejaa amani na utulivu.

Dr. Kyongo aliendelea kusema uzalendo ndiyo unaosababisha amani kwenye nchi yeyote na kumshukuru, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan kwa kuzidi kuifanya nchi izidi kuwa amani na utulivu kwa uongozi wake bora.

Dr. Kyogo alitumia nafasi hiyo kulishukuru Jeshi la Polisi nchini kwa kusimamia usalama wa watu na mali zao kuanzia kwa afande IGP Simon Sirro, Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Murilo Jumanne, Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi wa Ilala, Debora Magiligimba na wasaidizi wao wote.

Washiriki wengine walioshiriki jogging hiyo kama wanajamii ni Mkufunzi wa Chuo cha Ustawi wa Jamii, Dr. Nuru, Askari Jamii, Wafanyabiashara na wakazi wa maeneo hayo.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii