Martin Fayulu aanza maandalizi ya uchaguzi wa mwaka 2023

Mwanasiasa wa upinzani nchini DRC, Martin Fayulu, ameanza maandalizi ya kuwania urais mwaka ujao baaya kongamano la siku tatu ya chama chake cha ECIDE mjini Kisangani.


Fayulu ambaye mwaka 2018 aliwania urais wa DRC na kushindwa na kiongozi wa sasa Felix Thisekedi, ameushtumu uongozi ulio madarakani kwa kuyumbisha uchumi na kushindwa kuwahakikishia usalama wakaazi wa Mashariki mwa nchi hiyo.

Baada ya kongamano hilo mjini Kisangani, Fayulu amekuja na ahadi anazosema angependa kutekeleza iwapo atachaguliwa kuwa rais wa nchi hiyo mwaka ujao.

Fayulu sasa akiwataka raia wa DRC kumchagua katika uchaguzi wa mwaka ujao, akiahidi kutatua changamoto zinazowakabili hasa utovu wa usalama mashariki mwa taifa hilo.

Katika kongamano hilo Fayulu amesisitiza umuhimu wa kuuda muungano wenye nguvu aliosema utamsaidia kungia madarakani huku akiendelea kudai kuwa aliibiwa katika uchaguzi wa  mwaka 2018 alipowania chini ya vuguvugu la Lamuka.

Haya yanajiri wakati huu Mahakama ya juu nchini humo tarehe 21 mwezi huu ikitrajiwa kuamua iwapo itamfungulia mashtaka ya ufujaji wa mamilioni ya dola fedha wa umma aliyekuwa waziri mkuu Augustin Matata Ponyo, na watu wengine wawili, wakati alipokuwa katika nafasi hiyo , madai anayokanusha na kutaka Mahakama hiyo kutoendelea na kesi hiyo.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii