MAPACHA WATOROKA NYUMBANI KISA KUPELEKWA SHULE TOFAUTI

Familia moja katika mtaa wa Rupingazi Mji wa Embu imejawa masikitiko na uchungu kufuatia kutoweka kwa watoto wao pacha wenye umri wa miaka 15.
Leon Macharia na Ryan Mwenda, waliokuwa kidato cha pili katika Shule ya Upili ya Moi Mbiruri na Shule ya Upili ya Wavulana ya Kangaru, mtawalia, walitoweka nyumbani walipokuwa wakijiandaa kuripoti shuleni mnamo Jumanne, Julai 12 alasiri.
Mama yao, Naisera Muthoni, alisema kwamba wawili hao waliacha sare zao na mikoba ya shule.
Muthoni alisema wanawe hawakuwa na masuala ya utovu wa nidhamu ila wasiwasi wao pekee ni pale walipotenganishwa wakiwa shule ya upili.
Mwanamke huyo alisema suala hilo liliibuka tena wakati wa likizo, lakini alilidharau, bila kujua kuwa linaweza kuwalazimisha wanawe kutoroka nyumbani.
"Walituuliza mara kwa mara kwa nini tuliwapeleka katika shule tofauti swala ambalo wenzao pia walikuwa wakiwauliza mbona walikubali kutenganishwa," Muthoni alisema kwa uchungu.
Muthoni alisema waliazimia kuwasajili wawili hao katika shule tofauti ili kuwawezesha kukuza maosha yao kibinafsi tangu wakiwa pamoja walipozaliwa.
Alisema wawili hao walikuwa na KSh 2,000, ambazo alikuwa amewapa kutumia shuleni.
Mama huyo mwenye huzuni sasa anaomba usaidizi wa kuwapata wawili hao. Yeyote aliye na habari kuwahusu anaweza kumfikia kupitia kwa nambari 0723511745 na baba yao, Joseph Mwaniki, kwa nambari 0722321655.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii