Urusi inazituhumu nchi za magharibi kwa kuwahami wanajeshi Ukraine

Wizara ya mambo ya kigeni ya Urusi, imeyatuhumu mataifa ya Marekani na Uingereza kwa kuwapa mafunzo wanajeshi wa Ukraine, Urusi ikitaja hatua hiyo ya mataifa ya NATO kama vita vya kutumia habari za uwongo dhidi yake.


Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari, Maria Zakharova, msemaji wa wizara hiyo ameeleza kuwa Washington imewatuma wataalam wanaowafunza wanajeshi wa Urusi kutumia silaha za hali ya juu zilizotengenezewa nchini Marekani.

Taarifa hiyo inasema kuwa wanajeshi wa Ukraine wameonekana wakitumia roketi zenye uwezo wa kutekeleza mashambulio ya mbali zaidi zinazoaaminika kutumiwa na Marekani.

Zakharova anaeleza wanajeshi wa Kyiv kwa usaidizi wa wataalam hao wa Marekani wamekuwa wakitumia roketi hizo kushambulia makazi ya raia katika maeneo yanyokaliwa na vikosi vya Urusi.

Mataifa ya Ukraine na Urusi yameendelea kukana madai kuwa yanawalenga raia katika vita hivyo ambavyo vimeshuhudiwa kwa miezi mitano sasa.

Awali Marekani ilikuwa imesema kuwa roketi nane zenye uwezo mkubwa zitaanza  kutumika nchini Ukraine katikati ya mwezi Julai.

Wataalam wa masuala ya kijeshi wanaamini kuwa silaha hizo huenda zikabadili mkondo wa vita vya Ukraine na Urusi, Kyiv nayo ikisema kuwa tayari imetumia roketi hizo kuharibu baadhi ya silaha za jeshi la Ukraine mashariki mwa taifa lake.

Zakharova pia akikashifu mpango wa Uingereza wa kutoa mafunzo kwa mamia ya wanajeshi wa Ukraine kutumia silaha jijini London.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii