Marekani inasema imemua mmoja wa viongozi wa IS nchini Syria

Marekani inadai ushindi mwingine dhidi ya kundi la Islamic State, ikisema ilimsaka, kumlenga na kumua mmoja wa viongozi wa tano wa ngazi ya juu wa kundi hilo la kigaidi, wakati wa shambulio la ndege isiyokuwa na rubani kaskazini magharibi mwa Syria.

Uongozi mkuu wa jeshi la Marekani mashariki ya kati (CENTCOM) umemtambulisha afisa huyo mkuu wa Islamic State kama Maher al-Agal, ukimuelezea kama kiongozi wa tawi la IS huko Syria na kama kiungo muhimu kati ya kundi la IS na washirika wake duniani.

“Al-Agal alikuwa na jukumu la kuimarisha maendeleo ya mitandao ya ISIS,” CENTCOM imesema katika taarifa.

Katika taarifa Jumanne, Rais wa Marekani Joe Biden alipongeza shambulio hilo kwa kutuma “ujumbe mkali.”

“Kifo cha Al-Agal kimemuondoa uwanjani gaidi mkubwa na kimepunguza vya kutosha uwezo wa ISIS kupanga, kupata uwezo wa kifedha na kuendesha operesheni katika eneo hilo,” Biden alisema.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii