Waasi washambulia kusini/mashariki mwa Ethiopia

Maafisa wa serikali ya Ethiopia wamesema waasi wameushambulia mji wa kusini/mashariki wa taifa hilo wa Gambella na kusababisha makabiliano ya risasi yaliodumu kwa masaa kadhaa hadi vikosi vya usalama vilipofanikiwa kuidhibiti hali.Mashambulizi hayo yanadaiwa kufanywa na wapiganaji wa kabila ya Oromo (OLA) ambao wana nguvu katika jimbo la Oromia, kundi ambalo serikali ya Ethiopia inalitaja kuwa ni la kigaidi.Waasi wa OLA mwaka jana waliungana na wapiganaji wa Tigray (TPLF), ambao wamekuwa katika mzingiro wa jeshi la Ethiopia tangu Novemba 2020.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii