Bunge la Japan limepitisha mswada wa sheria mpya ya kudhibiti matusi mitandaoni ambayo inatarajiwa kusainiwa na Rais wa nchi hiyo ambayo inatoa hukumu ya mwaka mmoja jela au faini ya Yen 300,000 ambayo ni sawa na dola 2,200.
Sheria hii ni marekebisho ya sheria iliyopita kuhusu masuala ya udharirishaji na matusi mitandaoni ambayo ilikuwa inatoa adhabu ya kuzuiliwa kutumia huduma hiyo kwa muda wa siku 30 pamoja na faini ya Yen 10,000 ambayo ni sawa na dola 75.
Mswada huo umeleta mgawanyiko wa mawazo na mitazamo miongoni mwa wananchi wa Japan baadhi wakisema kuwa itazuia uhuru wa kuongea na kujieleza na wengine wanaoafiki wakisema itasaidia kupunguza udharirishaji na matusi ya mitandaoni.
Kwa mujibu wa Msemaji kutoka Wizara ya Sheria, sheria hii ya matusi mtandaoni inatofautiana na sheria ya kumchafua mtu (Defamation).
Mwanasheria wa makosa ya jinai kutoka nchini Japan Seiho Cho ameonya kuwa sheria hii mpya haitoa ufafanuzi ni lipi hasa kosa linalotafsiriwa kama udharirishaji.
“Kulikuwa na ulazima wa kuwepo muongozo unaothibitisha lipi ji tusi.
“Kwa mfano kwa sasa kama atatokea mtu akamuita kiongozi wa Japan mjinga, pengine kwa sheria hii mpya iliyofanyiwa marekebisho inaweza kutambulika kama tusi.” Alisema Cho.