Zelensky ataka nguvu ya Ujerumani katika vita vyake na Ukraine

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky ametoa wito kwa Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz kuchukua msimamo ulio wazi zaidi katika mzozo wa taifa lake na Urusi.Akizungumza na kituo cha televisheni cha Ujerumani cha ZDF amesema wanataka kansela Scholz kutoa hakikisho la uungaji wake mkono kwa Ukraine. Na kuongza kuwa yeye na serikali yake lazima wafanye uamuzi.Rais huyo amesema lazima Ujerumani ijaribu kuweka uzani katika uhusiano wake na Ukraine na ushirika wake na Urusi. Amesema ukweli wa wazi ni kwamba Ujerumani ilianza kutoa suilaha kwa Ukraine kwa kuchelea kuliko majirani na taifa hilo. Katika hatua za awali za vita vya Ukraine na Urusi, Ujerumani na Ufaransa zilielezwa kuunga mkono Ukrained kisiasa na kwa mazungumzo.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii