Watu kadhaa wauawa na maelfu kuyahama makazi yao kufuatia shambulio

Nchini Burkina Faso, watu wenye silaha waliwashambulia wakazi wa eneo la Seytenga, karibu na mpaka na Niger usiku wa Jumamosi Juni 11 kuamkia Jumapili Juni 12, shambulio ambalo ni la kulipiza kisasi na ambalo lilifuatia shambulio dhidi ya kikosi cha jeshi la wilaya hii siku ya Alhamisi, Juni 9.


Hakuna idadi rasmi ya vifo na majeruhi iliyotangazwa kwa sasa lakini vyanzo kadhaa vinabaini kwamba watu kadhaa waliuawa. Idadi kubwa yavikosi vya usalama na jeshi vimetumwa katika eneo hilo, kulingana na msemaji wa serikali.

Kulingana na mashuhuda, watu wenye silaha wamekuwa wakiwahangaisha watu huko Seytenga kwa siku kadhaa. Baada ya shambulio dhidi ya kikosi cha jeshi siku ya Alhamisi, Juni 9, vikosi vya jeshi vilikuja kusaidia na vilifanya operesheni moja ya kijeshi katika eneo hilo. Walifanya opereshi yao hioyo katika mjiwa Dori kwa kushirikiana na polisi.

Kulingana na serikali, watu hawa wenye silaha walivamia mji wa Seytenga kushambulia raia. Washambuliaji walikuwa wengi, kinasema chanzo cha usalama". Waliua kila mtu waliyekutana naye,” amesema mkazi wa eneo hilo.

Hakuna idadi inayoweza kutolewa kwa sasa, "kwa kuzingatia jinsi hali ilivyo," kulingana na msemaji wa serikali.

Hali hii imesababisha wakazi wa wilaya hii kuhama na kuelekea mji wa Dori, takriban kilomita arobaini. Majeruhi walipelekwa katika vituo vya afya kwa matibabu.

Zaidi ya wakaazi 2,000 walianza kuondoka katika mji huo siku ya Ijumaa baada ya vikosi vya usalama kuondoka na kisha kwa sababu watu wenye silaha walirudi kushambulia mji huo, kulingana na afisa aliyechaguliwa wa eneo hilo.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii