Mafuriko yasababisha maafa mjini Sydney

Maeneo mengi ya mji wa Sydney yamefunikwa na maji kutokana na mafuriko yaliosababishwa na mvua kubwa ilionyesha katika mji huo mkubwa zaidi nchini Australia. Maji yenye kina cha mita 1.5 yamevizingira baadhi ya vitongoji vya mji huo huku idara ya dharura katika jimbo la South Wales uliko mji wa Sydney, imetoa tahadhari kwa wakaazi wa jimbo hilo kuyahama makaazi yao na kuonya kuwa mvua inatarajiwa kuendelea kunyesha hadi kesho Jumatatu. Kwa mujibu wa vyombo vya habari mjini Sydney, mvua ilionyesha katika eneo hilo ni mara nne zaidi ya kiwango cha kawaida kwa mwezi Julai. Hata hivyo mamalaka ya hali ya hewa nchini Austaria iliwahi kuonya kuwa viwango vya maji katika eneo hilo vinaweza kupanda huku sehemu za mabondeni zikitarajiwa kuwa katika hali mbaya zaidi.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii