Jeshi la Sudan lafyatua mizinga eneo la mpaka na Ethiopia

Wanajeshi wa Sudan wamefyatua mizinga wakati wa makabiliano katika eneo la mashariki lilalozozaniwa ambalo linapakana na Ethiopia. Hayo ni kwa mujibu wa afisa mmoja wa Ethiopia, ikiwa ni tukio la hivi punde katika mzozo wa muda mrefu kuhusu mpaka wao wa pamoja. Afisa wa jeshi la Sudan ambaye hakutaka kutajwa jina lake kwa sababu hana ruhusa ya kuzungumza na vyombo vya habari amesema Sudan jana ilifanikiwa kulikamata eneo la Jabal Kala al-Laban, lililo karibu na mpaka huo unaogombaniwa kufuatia mashambulizi ya mizinga na shambulizi la kutokea angani. Assefa Ashege, afisa mwandamizi wa usalama katika jimbo la Amhara la Ethiopia amesema jeshi la Sudan lilifyatua mizinga ya masafa marefu kuanzia Jumatatu asubuhi hadi jana mchana, lakini hakuna aliyeumia. Ethiopia ilikanusha Jumatatu tuhuma za Sudan kuwa jeshi lake liliwakamata na kuwauwa wanajeshi saba wa Sudan na raia mmoja, na badala yake kusema mauaji hayo yalifanywa na wanamgambo wa eneo hilo.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii