Miss Bbrazil 2018 Afariki Baada ya Kufanya Upasuaji

Gleycy Correia ni aliyekuwa Miss Brazil mwaka 2018 ambaye amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 27 baada kufanyiwa upasuaji (sajari) kutoa mafindofindo.

Kwa mujibu wa vyombo vingi vya habari vya kimataifa, mrembo huyo aliyefariki dunia Juni 16, mwaka huu alipatwa na kiharusi na mshtuko wa moyo baada ya upasuaji huo ambapo alitokwa na damu nyingi.

Gazeti la The Sun linaripoti kuwa mrembo huyo alikaa kwa takriban miezi miwili kwenye moja ya hospitali nchini Brazil akiwa hajitambui baada ya upasuaji.

Mrembo huyu anadaiwa kukaa Hospitali kwa muda wa miezi Miwili bila kujitambua kabla ya kukutwa na mauti

Taarifa hiyo pia imetolewa na familia ya mrembo huyo.

Kiongozi wa kidini ambaye ni rafiki wa familia ya mrembo huyo, Mchungaji Jak Abreu ameeleza uchungu wake kwenye mitandao ya kijamii.

Abreu anafichua kuwa wazazi wa mrembo huyo wanaamini kuwa kulikuwa na uzembe wa kimatibabu katika upasuaji wake.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii