Maafisa polisi wawili wameuawa kufuatia shambulizi lililofanywa na wanajihadi huko Benin

Maafisa wawili wa polisi waliuawa na mmoja kujeruhiwa katika shambulizi dhidi ya kituo cha polisi kaskazini magharibi mwa Benin siku ya Jumapili duru za polisi zilisema.

Mashambulizi ya karibuni katika msururu wa mashambulizi mabaya katika jimbo lililoathiriwa na harakati za wanamgambo katika nchi jirani za Burkina Faso na Niger. Watu wanaoshukiwa kuwa wapiganaji wa kiislam walivamia katika kituo cha polisi cha Dassari majira ya saa nane alfajiri na walifyatua risasi na kuwaua maafisa wawili kabla ya kurudishwa nyuma alisema afisa mmoja wa polisi ambaye hakutaka jina lake litajwe.

“Polisi wetu walifanikiwa kupambana. Kwa bahati mbaya kulikuwa na watu wawili waliokufa katika safu yetu” afisa wa polisi aliliambia shirika la habari la Reuters. Magaidi wawili pia waliuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa aliongeza.

Afisa wa pili wa polisi ambae hakutajwa jina pia amethibitisha shambulizi hilo pamoja na idadi ya vifo. Dassari ni mji uliopo kilomita 600 sawa na maili 373 kaskazini-magharibi mwa Cotonou mji mkuu wa Benin karibu na mpaka wa Burkina Faso.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii