NYANI WAVAMIA MAKAZI YA WATU

Kundi la nyani wa hifadhi ya Gombe iliyopo kijiji cha Mwamgongo wilayani Kigoma, limevamia nyumba ya Shayima Faya (20) na kumpokonya mtoto mchanga wakati akimnyonyesha na kutokomea naye porini ambapo baadaye mtoto huyo alifariki dunia.

Akizungumza leo Jumatatu Juni 20, 2021 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma, James Manyama amesema tukio hilo limetokea Juni 18, 2022 katika kijiji hicho.

Amesema baada ya tukio hilo mwanamke huyo alipiga kelele  kuomba msaada na majirani walijitokeza kumdhibiti mnyama pori huyo ambaye alimtupa mtoto huyo chini akiwa tayari amejeruhiwa kichwani, usoni na mguu wa kushoto.

"Wananchi walifanikiwa kulikimbiza kundi hilo la nyani lililomvamia mwanamke huyo wakati akimnyonyesha wanaye,  na kufanikiwa kumpata mtoto akiwa amejeruhiwa lakini baada ya kufikishwa kituo cha afya Mwamgongo alifariki dunia,"amesema Manyama.Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii